» » » » Zari Awapiga ‘Stop’ Ndugu wa Mwanamuziki Diamond Platnumz


Stop! Wakati akisubiriwa kujifungua muda wowote, mwandani wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anadaiwa kuwazuia baadhi ya ndugu wa jamaa huyo kuingia kwenye chumba maalum kilichoandaliwa ili kuepuka kisiingie vumbi na kiwe safi wakati wote.

Chanzo chetu ambacho ni mmoja wa ‘memba’ wa familia hiyo kilipenyeza kuwa, kwa sasa nyumbani kwa mwanamuziki huyo maeneo ya Madale-Tegeta, Dar, wana bashasha wakimsubiria mtoto huku chumba hicho kikiwekewa uangalizi mkubwa.
“Yaani Zari hataki mchezo kabisa na haruhusu mtu kuingia chumbani humo hovyo kwa sababu ya kuepuka vumbi kwa mtoto kwa maana chumba hicho hakihitaji msongamano wa watu wengi,” kilisema chanzo hicho.

Mpashaji huyo aliweka wazi kuwa, Zari alitia ngumu na kusema ni sheria aliyoiweka mwanamama huyo na haitakiwi kukiukwa na mtu yeyote kwa kuwa wanafahamu fika kuwa chumba cha mtoto hakihitaji msongamano wa watu hivyo ndugu hao imebidi wawe wapole.
Kilidai kwamba, kwa sasa kila mtu anayefika nyumbani hapo anahojiwa na kwamba kama siyo ndugu wa ndani zaidi kwenye familia haruhusiwi hata kuingia getini.Akizungumza na Ijumaa Wikienda kuhusu maandalizi hayo, Diamond alisema kila kitu kipo sawa na kwamba, anamuomba Mungu mambo yaende kama alivyopanga.

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply