TANZIA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeshi Kombani amefariki dunia
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani amefariki dunia nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu
Taarifa tulizozipata usiku huu zimesema kuwa Waziri Kombani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Ulanga Mashariki kupitia chama cha Mapinduzi, mwili wake utawasili nchini Jumamosi ya Septemba 26 mwaka huu
Mtandao huu unatoa pole kwa familia ya marehemu na taifa kwa ujumla kwa msiba huu.
No comments: